Saturday, August 4, 2012

Izzo Bizness ft. Belle 9 - Utarudishwa

Intro: Izzo Bizness

Attention!!!
This Is Dirty Mode Record and One The Incredible
I got ma big boy Belle 9
Mbeya City
Triss, Word Up
Is On TOP now, whooohh
Here we go now

Verse 1: Izzo Bizness

Mateso dhiki bado hadithi haijaisha, vya kurithi wamebinafsisha
Njaa adui mkubwa na silaha zimetuishia, tusaidieni nyie wakubwa tuliwachagua
Mpenzi tabu kazichoka na bado ananizimia, kachoka shona viraka wadau wanamvizia (woohhh)
Yataka moyo wapinzani kila kukicha, ubinafsi chuki na uchoyo argh kila kukicha
Viganja vinawasha na pesa haionekani, habari nawapasha tumtafute mchawi nani
Sio MBEYA dunia nzima wote tuingie vitani, Say what??
Dunia nzima wote tuingie vitani… whooh
Graph yangu ipo kasi inapanda hata haishuki, wanao-fake ni wafuasi sasa imefika tamati
Hawapindui hawajui wote kwangu ni masokolo, mimi msondo hawajui wao Twanga Chipolopolo

Chorus: Belle 9 & Izzo Bizness
Izzo… What??
Izzo… That’s Ma Name
Utarudishwa MBEYA
Izzo… what you saying
Izzo… Yeaaah
Utarudishwa MBEYA
Izzo… Na Naniii?
Izzo Izzo… Utarudishwa MBEYA
What??
Izzo… acha kuwabana, Izzo… kausha
Utarudishwa MBEYAAA
Shauri Yakooo




Verse 2: Izzo Bizness

Nawasoma uwezo hawana nawabana, nawamwagia zangu laana
Uzito wao bado mdogo kilo zetu hazifanani, siogopi kuwapa kisogo kusema wamseme nani
Haya kweli mapinduzi thanks a lot FA, hawanitishi hawa makuzi anga hizi hawasogei
Sitishiki na mizoga watishieni hao fisi, wanakesha wanaroga siogopi nawapa stress
Nawapuliza hawaenei wanahofia, wameanza mimi namaliza hii mvua nawanyeshea
Nawatwanga nawapepeta muulize Asha Baraka, melody tamu za matata mpaka utamu umepita
Movie hii sio bongo si-shoot kwa siku moja, nooh… mi ni star mwenye usongo uta-dead kwa hizi hoja
Wabunifu wa mavazi sikujua kumbe ma-model, hivi haikushangazi kwa IZZO ukileta nyodo…
Aaannhhh

REPEAT CHORUS:

Verse 3: Izzo Bizness

Yote wananisema mimi, siwezi loose nimejipanga isitoshe najiamini
Got image good looking yes ladies they love me, still roll and rocking and my hood still shining
Big contracts I keep on signing hommie, yeah nigga I keep on signing
Tamaa chanzo cha dhambi so vizuri tukaishinda, wanaobebwa hawatambi wanajiita mabingwa
Akili nguvu tele ninazo jipange kushindana, niite mjinga toa vigezo we mnyonyaji huna maana
Natubu kama Chiddi japo sitokei Ilala, nasema ukweli inapobidi na uniamini kama sala
Maisha ya shida na njaa ndio chanzo cha u-ganster, hii ni mtaa kwa mtaa kujichanganya tupo faster
UYOLE, MWANJELWA, SOWETO hawakatai, pande za ILOMBA, MBALIZI mpaka wanangu wa SAE
MAMA JOHN, ISANGA mpaka NONDE kwa makauzu, visu na mapanga ukionekana kavu
Uuuuuhhhhh

Clam down Bizness
Nani wa kunirudisha sasa
Calm Down

Lyrics: Stamina ft. Rich Mavoko - Najuta Kubalehe

INTRO
Rich mavoko:uooooooooooooo oooooooo annnnnhhhhaaa{x3}
Stamina;iz moro town baby,im back,u know wat kevy,this iz so matured meeeen

Verse 1 {stamina}
Shida zinaomba urafiki,umasikini unaleta posa
Ukubwa meli ya kigiriki,nimezamia bila boxer
Bikra ya utoto,imeshavunjwa na balehe
Ukubwa una mingi misoto,na mchanganyo wa starehe
Mara ooooh baba kijacho,eti niandae hela ya nepi
Wife anatoa macho,anangoja shopping ya sketi
Hakimu ana nyundo ya noti,mtuhumiwa nasaka chenchi
Bongo mahakama za joti,me mpoki nabaki benchi
Hata nikimchukia baniani,kiatu chake kina mchango
Mzinzi na nyota ya kijani,ndio uzazi usiokua na mpango
Balehe noma,kama baunsa aliyepigwa na mtoto
Ukubwa mechi ya kisodoma,haiwezi chezeshwa na mpoto
Aaaaah kas na kas,ni kasi isiyokua na kasi
Ila nikiweka kas na kus,ndio kusi pacha wa kasi
Bora wewe jalala,me ukubwa shimo la choo
Ukichanganya na ufukara,ndio mechi isiyokua na droo

Chorus {rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe

Verse 2 {stamina}
Maisha ngumi ya bitozi,siogopi kutega sura
Pesa sitafuti kwa pozi,bado najinyima kula
Nishachoka kusadiki,tomaso tangu na tangu
Marafiki wanafiki,wanasnitch hadi kwa mke wangu
Majukumu ya familia,nimeyabeba bila ngata
Asili zimezidi mia,desturi zimenikamata
Haya maumivu ya mjeledi,kwenye ngozi ya mlemavu
Ukubwa mechi ya mabaamedi,me mlevi nafungwa kavu
Aaaah maisha jabali,ugomvi wa cheka na Tyson
Sikuhizi ukinunua hata kagari,kitaani unaitwa free mason
Maumivu ya sufuria,jikoni hayana ushuru
Pesa tajiri wa dunia,mwenye hisa yangu ya uhuru
Aiseh sayansi imenikera,ukuaji umenipa msoto
Utu uzima bila hela,utamwamkia hadi mtoto
Napopata mkwanja,na shida zinagonga hodi
Vipi nitanunua kiwanja,huku bado nadaiwa kodi

Chorus {rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe

Verse 3{stamina}
Ukubwa msafara wa kenge,me mjusi vipi unichoshe
Penzi kitovu cha uzembe,nakaza nisiitwe ngoswe
Ugangstar bila hela,majibu yake ni uchafu
Maisha ya bongo msosi wa jela,so mfungwa usiulizie ndafu
Nilizoea kashata,bumunda na vibagia
Huku unga,bangi,na bapa,ndio vitu navyovisikia
Chuki na fitina,hadhina za wenye wivu
Wapo wanaonishirikina,ili moto nigeuke jivu
Udogoni nilidekezwa,wazazi walinipa malezi
Pesa imesomea udereva,inaendesha hadi mapenzi
Elimu ya njia za panya,inanikosesha michongo
Madeni yananiandama,kama serikali ya bongo
Maishani ukiwa govinda,wenzako watakuita yaya
Pesa mnyama anayewindwa,na jangiri aliyevuta kaya
Uwazi unanidondosha,bado narushiwa kombora
Condom ndio kinga tosha,sijikingi na bastora

Chorus {rich mavoko}
Kama nakufuru,mungu naomba unisamehe
Nakosa uhuru,sikumbuki hata tarehe
Kweli najuta kuzijua hizi starehe eeeeeee eeeeeee eeeeeee eeeeeehh
Ehhhh me najuta kubalehe
Ehhhh sikumbuki hata tarehe
Eeee ujana maji ya moto,zinaniunguza hizi starehe
Bridge{rich mavoko}
Heri ningerudi utoto,ujana maji ya moto
Eeeeeeeeh eeeeeh eeeeeeeh eeeeeeeehhh
Me najuta kubalehe,me najuta kubalehe eeeeeeh,me najuta kubaleeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhh

Ontro {stamina}
Moro in da house,in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Moro town in da house,stamina in da house
Ahahaha I luv hip hop