Tuesday, July 17, 2012

Fid Q ft. Yvonne Mwale - Sihitaji Marafiki





Verse 1.

Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani/
Udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani X2/
Haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao,
Washkaji ambao kosa lako lao wakati hauna mafao/
Wanaokufikiria wewe muda ambao/
Wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao/
Now
Kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi/
Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi Sihitaji urafiki na usupastaa/ukihit ndo unang'aa
Upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../
Kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground/
Sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau/
Wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
Ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza/
U-N-I-T na Prof. Ludi walionifunza kukaza
Kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea


Verse 2;

Na usupastaa huwa ni feki... utakung'arisha ukiwa na Market/
Utakupatia senti,utapita juu ya red carpet/
Utageuka young & restless, utakupa wanawake/
Utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake/
Kwahiyo power is not permanent.. huwa ipo kwa muda tu/
Respect your own conglomorete... fikiri kikubwa tu/
Masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu
Walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru/
Wanazusha najiskia.. so im my own best friend/
Sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/
Naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship/
Tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/
Na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea


VERSE 3

Rafiki wa kweli yukoje... ni mkimya au anayechonga/
Yule aliyekupa jina?au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?/
Au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ Hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/
Bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe/
Ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?/
Kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo/
Inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/
Unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/
Urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo/
Nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature/
Wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger/
Sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

Godzilla ft. Marco Chali - Nataka (Produced by Marco Chali


Verse I
Weita leta mitungi ,
Mbaka asubuhi nakunywa siyumbi(X2)
Nipe mimi pia na marco chali,
Usijari nje nimecome na gari
Vumbi linatimKa basi njoo uone
Kwasa kwasa mbaKa zile indemonie
Mambo yako poa kila kitu mukide mukide,
Ka dully juu chini mwendo shikide shikide
Beef cha yupo na wolper
Kwenye viwanja zilla huwezi nikosaa

(Bridge)
(Nasema ahahahah
Ayaaayaa yaayaaa)X2

Chorus:
NataKaaa,kusomeka viwanja vyote na sehemu,
Zenye baata,
Cheza na manzi yangu lakini usivukee mipakaa,
Ukijifanya mtoto wa mbwa si wenyewe mbona watoto wa paKa.
Ahaahah(hahaah)

Verse II#
Dondoshaa champgne again
Counter nimeclear,niko safi sina deni(X2)
Watoto wamepandishaa moriii
Hizi ndo zetu tukikuuzi we sorry
Hapa ni tungi badala ya tungi
Usiku mzima busy tunasaga mirungi
Mkono wa kushoto big g na soda.
Nahitaji john walker nimeshaweka order,
Angushaa hiloo bapa here we go
Tungi haliishi zimejaa kwenye store

(Bridge)
(Nasema ahahahah
Ayaaayaa yaayaaa)X2

Chorus:
NataKaaa,kusomeka viwanja vyote na sehemu,
Zenye baata,
Cheza na manzi yangu lakini usivukee mipakaa,
Ukijifanya mtoto wa mbwa si wenyewe mbona watoto wa paKa.
Ahaahah(hahaah)

Bridge:
Nipo nipo kwenye party
We unabaki hapa mi nasonga palee
(X2)
Leta leta ,letaa mondee letaaa
Leta leta letaa mondee basi letaa

Chorus:
NataKaaa,kusomeka viwanja vyote na sehemu,
Zenye baata,
Cheza na manzi yangu lakini usivukee mipakaa,
Ukijifanya mtoto wa mbwa si wenyewe mbona watoto wa paKa.
Ahaahah(hahaah)


Click To Listen 

Wednesday, July 11, 2012

AY ft. Marco Chali - Party Zone


Intro:
Marco:
Skia hii ndio fact usiact like you don't know
The way u treated me ulishanipa somo
Skia hii ndio fact usiact like u don know
The way u treated me ulishanipa somo

AY:
Verse 1:
Uliniona sifai,
Ukaniacha ukaenda mbali,
Dunia imekuonyesha
Sa unataka hurudi NO
Maisha haya safari
Uliniacha wakati nakuhitaji
All I wanna do
Niziache stress zi GO................

Dance tonight,
Drink tonight,
Smoke tonight,
Nijipe raha tuu....
Nihave fun tonight
Cruise tonight
Blast tonight
/stress zigoooo

CHORUS:

Party Zone x8

Marco:
Skia hii ndio fact usiact like you don't know
The way u treated me ulishanipa somo
Skia hii ndio fact usiact like u don know
The way u treated me ulishanipa somo

AY & Marco :
Hands up in the air (Pa x4 Party Zone)
Maumivu yashapotea (Pa x4 Party Zone) x2

AY
Maisha yanasonga naishi simple
Siku zinakwenda nishatua mzigoo
Yale uliyonitendea nishajiondoa kwako
Long time nishajiondoa nawaachia tu hao nishaanza new life

Marco:
Uliniacha without sayin bye
Ulini-fa-nya niumie
Maumivu yote kwangu yashafly
Nipe nafasi nijiachieee

AAAAAAYYY,CHA CHA CHALLLLIII!!!!

AY:
Niache nienjoy my life
Nawe enjoy ya' life
Sleep all day Up all night
Nishazoea New Life
Huna tena nafasi
Niache nienjoy my life

Party zone x8

AY:
Zile pain/damages/dharau/kebehi/attitude
Zinanifanya moyo wangu usitamani kabisaa yaani we hurudi
\so nahitaji space
Nafasi yako ishawekwa desh
Handle ya' business
Before ya' business handles you
/wacha mi nienjoy tu
Kinyume cha pain (happy tu)
Maumivu tupa kule
#i'm happy now#

Dance tonight,
Drink tonight,
Smoke tonight,
Nijipe raha tuu
Nihave fun tonight
Cruise tonight
Blast tonight
/stress zigoooo

Party Zonex8

Maisha yanasonga naishi simple
Siku zinakwenda ni shatua mzigoo
Yale uliyonitendea nishajiondoa kwako
Long time nishajiondoa nawaachia tu hao nishaanza new life

CREDITS:

AY Featuring MARCO CHALI
PARTY ZONE
MJ RECORDS

GODFATHER PRODUCTION


You also need to see the Video sound if you didn't... DOPE!!!
AY take us there!

Tuesday, July 10, 2012

MwanaFA ft. Dully Sykes & AY - Ameen

Intro:
Ni MwanaFA
Yupo na Dully Sykes
Silent Ocean
Inna Mi Yard
Keeping The Good Music Alive
Yessayah

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 1: MwanaFA
Ziende,on and on kama Eryka Badu/wafahamu sababu/ni heshima kwa Mungu/
Natembea kifua mbele yote sababu ya wewe/wote wanaojipindua mwisho wanasanda wenyewe/
Binamu yangu Masumbuko ananisikia hata akiwa jela/jinsi nakinukisha na bado juhudi na sala/
Naomba hekima za Suleiman/sio miguvu ya bure/hata kauli zangu ndogo zionyeshe nilienda shule/
Maadui wafunge mikono nimewazidi wape ishara/wape akili za hasara wachezee kazi na mshahara/
Ikidunda sana inakaribia kupasuka/yangu ikeshe isiishe leo hata wajukuu wanaikuta/
Bora kuchekwa kuliko kuchekwa sana wanaonipinga waumize,Mungu nakomba sana/
Uwape umri mrefu wa kwangu na wa babu yangu/ili roho zao ziumie wakiona mabalaa yangu/Amen..

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 2: MwanaFA
Nisichokijua hakiwezi kunisumbua/wakisema mabaya yashindwe kunifikia/
Wape kismati cha paka cha kupendwa na wachawi/mi naomba cha pesa na kwa ujinga niwe kiziwi/
Wape wanawake wazee na mafukara halafu wagonjwa/ama mabwana mabwabwa wasiogonga kabla ya kugongwa/
Wanaomba nisiwe na kitu ili niombe waninyanyase/dhiki inijae vyote vya kwangu wavipate/
Kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe/kama wanichukue msukule nisionekane wabaki wenyewe/
Naishi kwa kudra,baraka,matakwa yako/siwezi nikachemsha kama ukibaki upande nilipo/
Competition is irrelevant/with you by my side/nafanya siongei na wanajua mi ni mastermind/
Haraka zaidi yao/uchungu zaidi yao/ukubwa au udogo wa tatizo unaletwa na akili zao/it's a wrap

Chorus:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee

Bridge:
Mi nna haraka zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/

END!

The Track is in reggae/riddim genre done by Dully's new studio known as "Dec 4th Studios", some tight lyrics from yo cousin AS USUAL!! Let Your Ears hear this. Yo' Boi deserves some credits...

Holla @ me with ya comment down below. One!

Brand New Track: C-Low ft. Rich Mavoko


Monday, July 9, 2012

Ben Pol - Number One Fan


Verse 1: Ben Pol
Nimeamini raha ya upendo ikipotea huwa karaha,
Sikutaraji kama leo hii nitabaki na jeraha,
My number one fan, tatizo ni wewe umefanya anitose
Wakati bado nampenda nafsi imejawa upendo wake x 2
Sikujua dhamira iliyokufanya we uwe karibu nami
Nafsi inanisuuta kwa kumkwaza hana hata raha moyoni
Alidai anaenda ili atuache mimi na wee
Na mi sitaki kupoteza penzi lake nifanyejee

Chorus
You just my number one fan
She is the one and I love her
She is everything in ma life
My dreams depend on her x 2

Verse 2: Ben Pol
Mi sijui hata nini nitafanya maana mpenzi hutaki nielewa
Ninakuomba kwa mara nyingine tena nisemehe we ndo nakupenda
Mwanzoni alidai anapenda nyimbo zangu jinsi navyoimba
Akasema angefurahi angepata muda wangu ajifunze kuimba
Kumbe nia yake haikiuwa vile mi nilivyodhania
Kumbe shida yake ilikuwa ile mpenzi ulivyonambia
Kumbe nia yake haikiuwa vile mi nilivyodhania
Kweli shida yake ilikuwa ile mpenzi uliyonambia
Sasa najutia ubishi wangu mimi na kukupuzia
Eti nisahau kuhusu wewe sababu yupo yeye ndivyo alivyonitamkia x 2

Chorus
You just my number one fan
She is the one and I love her
She is everything in ma life
My dreams depend on her x 4